Huduma za mtandao wa intaneti zimerejea kote nchini Sudan kufuatia amri ya mahakama iliyotolewa siku ya jumanne, wiki kadhaa tangu watawala wa kijeshi walipozima huduma hiyo wakati wa operesheni katili ya kuvunja maandamano ya umma.
Amri hiyo ya mahakama inafuatia shauri lililofunguliwa na mwanasheria mmoja wa mjini Khartoum aliyeitaka kampuni ya simu ya Zain iamriwe kurejesha huduma ya intaneti kwenye simu yake.
Huduma za intaneti zilizimwa kote nchini Sudan baada ya wanajeshi kuwatawanya kwa nguvu waandamanaji waliopiga kambi nchi ya makao makuu ya jeshi kushinikiza watawala wa kijeshi kuwachia madaraka.
Waandamanaji na makundi ya haki za biandamu wamesema kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti lilikuwa jaribio la watawala wa kijeshi kuzuia mipango ya kuhamasisha maandamano zaidi nchini humo.
0 Comments