Windows

Azam FC kusheza na Mabingwa wa Ligi kuu ya Burundi


Kikosi cha Azam FC kesho kitashuka Dimbani kwenye mchezo wa kitaifa wa kirafiki dhidi ya Aigle noir FC ambao ni mabingwa wa Ligi kuu ya nchini Burundi. Mchezo huo utachezwa saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Kocha msaidizi wa Klabu hiyo Iddi Cheche amesema kuwa mchezo wa kesho ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mechi za kimataifa na Ligi kuu Tanzania bara na kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye michuano ya KAGAME CUP.

"Mechi kesho ipo tutacheza saa moja usiku,lakini ni sehemu ya maandalizi yetu kwa ajili ya mechi zetu za kimataifa na Ligi kuu, mchezo wa kesho utakuwa na uzito kwa kuwa wale ni mabingwa wa Burundi hivyo uzito upo na yale mapungufu yaliyojitokeza kwenye KAGAME CUP tumeyafanyia kazi hizi siku tatu na hiki kitakuwa kipimo cha mechi zetu za kimataifa tutakazo cheza,"  alisema Cheche.

Post a Comment

0 Comments