Baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amepoteza  sifa za kuendelea kuwa mbunge, Lissu amesema atakwenda mahakamani.

Lissu amesema hayo usiku wa Ijumaa, akiwa Ubelgiji, amesema tangu aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa Area D jijini Dodoma Septemba 7, 2019 amekuwa akipata matibabu nje ya nchi.

Amesema kwa hatua ya sasa, “Nitawasiliana na wanasheria wangu haraka iwezekanavyo ili kuona cha kufanya lakini Septemba 7 (mwaka huu) ambayo nilikwisha kusema nitarudi   sitabadili, nitarudi na alichokifanya Ndugai ni kukoleza mjadala.”

Juni 28, 2019 (jana), Spika Ndugai ameliambia Bunge hilo kuwa amewandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kipo wazi.