KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘TaifaStras’ leo kimeondoka nchini Tanzania na kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi maalumu ya maandalizi ya michuano ya Afcon itakayofanyika nchini Misri, Juni 21.
Kocha wa Stars, Emanuel Amunike amesema kuwa amechagua timu yenye vipaji ambayo ana imani italeta matokeo kwa ajili ya Taifa la Tanzania.
“Vijana wengi wa Tanzania wana vipaji ndio ambao nimewajumuisha kwenye kikosi changu, wapo ambao nimewaacha na sababu kubwa ni kushindwa kuwa na nidhamu, pia wapo wale ambao walishindwa kutimiza mazoezi na wengine hawapo fiti.
“Najua kwamba kila mmoja anachaguo lake ila hamna namna ni lazima niwe na kikosi makini kitakachopambana, kwa vijana wadogo nimewajumuisha ili wapate uzoefu,” amesema Ammunike.
The post TAIFA STARS WAKWEA PIPA AFCON MISRI, WAAHIDI USHINDI – VIDEO appeared first on Global Publishers.
0 Comments