Rais Xi Jinping wa China  amekutana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni ambaye yuko ziarani nchini China. Marais hao wawili wamekubaliana kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa pande zote.

Rais Xi Jinping amesema China inapenda kushirikiana na Uganda, kutumia fursa ya ujenzi wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' na utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC, kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelezwa zaidi na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake rais Museveni, amesema Uganda inatumai kuzidisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali, kwa kutumia fursa ya kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa pande zote kati ya nchi hizo mbili. Amesema vitendo vya upande mmoja ni hatari, Uganda na China zinapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu katika mambo yanayohusu pande nyingi.