SHIRIKISHO la Soka barani (Ulaya) limetaja kikosi bora cha mastaa 11 waliong’ara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2018/19.
UEFA ilitangaza mastaa hao 11 bora muda mfupi kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Tottenham Hotspur iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid.
Straika wa Barcelona, Lionel Messi, ambaye amepachika mabao 12 kwenye michuano hiyo yumo katika kikosi hicho akiwa ametajwa kwenye safu ya ushambuliaji.
Sadio Mane, ambaye aliiongoza timu yake ya Liverpool kwenye mechi ya fainali dhidi ya Tottenham Hotspur jana, yumo pia kwenye listi hiyo ya wachezaji bora. Liverpool ndio imetoa wachezaji wengi zaidi katika kikosi hicho ikiwa imetoa watano.
Ajax Amsterdam ndio inafuatia kwa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye orodha hiyo kutokana na kuwa na nyota wawili. Kipa bora ni Alisson, ambaye ameng’ara na Liverpool msimu huu, huku mabeki wakiwa pamoja na Matthijs De Ligt (Ajax Amsterdam), Virgil van Dijk (Liverpool) na Andrew Robertson (Liverpool).
Wachezaji wa kiungo ni Georgio Wijnaldum (Liverpool), Benardo Silva (Manchester City) na Frenkie de Jong (Ajax Amsterdam). Wanaounda safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ni pamoja na Lucas Moura (Tottenham Hotspur), Messi na Mane.
ALI KIBA “NILIKUA Natamani ABDU KIBA Afunge MZUKA”
The post Messi, Mane Watajwa Kikosi Bora cha UEFA appeared first on Global Publishers.
0 Comments