Windows

Mbwana Samatta Awaniwa na Brighton, Aston Villa za England

 

 

Mshambuliaji wa Taifa Stars na Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anawaniwa na timu za England Brighton, Aston Villa kwa gharama ya Paundi Milioni 12 (Tsh. 34,930,999,680)

Pia Leicester, Watford na Burnley zote zimeonyesha nia ya kuitaka saini ya mshambuliaji huyo wa Genk.

Samatta (26), inafahamika kuwa anataka kuhamia England baada ya kuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta amefunga mabao 23 na kuisaidia Genk kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu huku yeye mwenyewe akitwaa tuzo ya Ebony Shoe inayotolewa kwa mchezaji bora wa Afrika anayecheza Ubelgiji.

Nyota huyo anafuata nyayo za Romelu Lukaku, Vincent Kompany na Michy Batshuayi.

Samatta ataiongoza Tanzania katika fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika baadaye mwezi huu nchini Misri.

The post Mbwana Samatta Awaniwa na Brighton, Aston Villa za England appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments