Maandamano ya vizibao vya njano yamefikisha wiki ya 33 nchini Ufaransa.

Wananchi wamekuwa wakiingia mitaani kumpinga rais wa sasa wa nchi hiyo Emmanuel Macron.

Kwa mujibu wa habari,maandamano hayo yameendeela licha ya kuwa na joto kali.Mjini Paris waandamanaji hao wametembea kutoka eneo la Clichy mpaka Porte de Pantin.Polisi walionyesha vurugu dhidi ya waandamanaji hao.

Wakati wa maandamano huko Lille na Rennes, polisi waliingilia kati na kumwaga risasi za machozi. Watu 18 huko Reims, 3 huko Rennes na 5 huko Lille wamefungwa.

Maandamano hayo yalianza nchini humo , waandamanaji wakidai  kukemea kupanda kwa bei za bidhaa mahitaji nchini Ufaransa.