Windows

Kisa Manara, Mobeto Ahofia Kubondwa

DAR ES SALAAM: Hivi karibuni mwanamitindo ambaye pia ni mwimbaji wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ‘Misa’, amekuwa karibu na Msemaji wa Timu ya Simba, Haji Manara na wamekuwa wakionekana pamoja kwenye mambo mbalimbali ikiwemo uwanjani.

 

Ukaribu huo umezua maswali mengi huku Mobeto mwenyewe akionekana kuhifia kubondwa kutokana na ukaribu huo.

Kufuatia ukaribu huo, Mobeto ameeleza hofu hiyo kupitia posti ya Manara kwenye Mtandao wa Instagram iliyowaonesha wakiwa pamoja.

 

Manara alipandisha picha hiyo Juni 2, 2019 na kuandika hivi; “Team Samatta tushampiga Kiba sita na baadaye tunafuturu kichampioni Serena Hotel.”

 

Kwenye posti hiyo baadaye Hamisa alikomenti kwa kuandika;

“Ipo siku utafanya tupigwe.”

Manara na Hamisa ambaye pia ni shabiki wa Simba, walikaa pamoja uwanja wa taifa na kutazama mechi ya Simba dhidi ya TP Mazembe na ile ya Simba dhidi ya Sevilla huku Manara akiweka picha zao mtandaoni hivi kuibua viulizo kila kona.

Stori: IMELDA MTEMA, IJUMAA

The post Kisa Manara, Mobeto Ahofia Kubondwa appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments