Kiungo Thabani Kamusoko jana aliupiga 'mpira mwingi' kwenye mchezo wa robo fainali kombe la COSAFA kati ya Zimbabwe dhidi ya Comoros, Zimbabwe ikiondoka na ushindi wa mabao 2-0
Kamusoko alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo
Baada ya mchezo Kamusoko alisema tuzo hiyo itamuongezea ari ya kupambana zaidi ili kuisadia timu yake kutwaa taji la CASAFA kwa msimu wa pili mfululizo
Mkongwe huyo amemaliza mkataba kunako klabu ya Yanga lakini bado anaonekana yuko vizuri
Kamusoko ana nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya Taifa ya Zimbabwe ambacho kitaelekea Misri kushiriki fainali za AFCON 2019
0 Comments