Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefanya shoo yake ya One man One Mic usiku wa Juni 5 katika uwanja wa Taifa mjini Kahama mkoani Shinyanga na kuwaacha mashabiki hoi baada ya kukiwasha kwa saa 5 (kuanzia saa 5 usiku hadi saa 10 alfajiri) bila kushuka jukwaani.
Akipiga story na wanahabari baada ya kumaliza shoo yake hiyo, Diamond amesema lebo yake ya WCB inafanikiwa siyo kwamba wanaroga kama baadhi ya watu wanavyodai mitandaoni badala yake wanafanya vitu vya tofauti vyenye ubunifu jambo ambalo huwavutia mashabiki zao.
Diamond ambaye leo atakuwa na shoo mjini Geita, amesema yupo mbioni kuimba wimbo wa miondoko ya Singeli kwa sababu uwezo anao na muziki unaopendwa sana kwa sasa hapa nchini.
MSIKIE DIAMOND AKIFUNGUKA
The post Diamond Afunguka: Sio Kwamba WCB Tunaroga, Nitaimba Singeli – Video appeared first on Global Publishers.
0 Comments