MAMBO yamemnyokea mshambuliaji wa Azam FC Obrey Chirwa baada ya kuelewana na kukubaliana kusaini mkataba wake mpya na klabu hiyo tukio ambalo litafanyika Jumamosi.
Awali Chirwa ambaye ni Mzambia ligoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na inatajwa kuwa malengo yake yalikuwa ni kutaka kurejea Yanga lakini kocha Zahera akamkaushia.
Chirwa aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kutimkia Misri kisha kurejea na kujiunga na Azam FC msimu huu katika ligi amefunga jumla ya mabao matatu.
Akizungumza nasi , Mratibu wa Azam FC, Philipo Alando alisema kuwa tayari wameongea na wachezaji kinachosubiri wa sasa ni kusaini tu na kuendelea na mambo mengine.
“Unajua kila kitu kina kwenda sawa Chirwa pamoja na wenzake tumeshaongea nao na kutakubaliana kilichokuwa kinasu biriwa ni wao kuweza kusaini mikataba yao na kundelea na mambo mengi,”alisema Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar na Azam.
0 Comments