


Baada ya kuwa na asilimia 100 za kuukosa ubingwa wa Ligi kuu msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa ni lazima wabebe ndoo hiyo msimu ujao.
Licha ya kumaliza katika nafasi ya pili, Zahera amesema timu yake imefanikiwa sana msimu huu kulingana na mazingira waliyokuwa nayo mwanzo wa ligi.
Pia amedai akiwa msimu wake wa kwanza Tanzania ameifahamu vizuri ligi kuu ya Tanzania aina ya wachezaji wanaohitajika na mbinu za kutumia msimu ujao.
"Tulianza kwa kuwa na malengo ya kumaliza nafasi ya sita au saba, lakini baada ya kuona tunafanya vizuri licha ya kuwa na changamoto nyingi, tukasema tujaribu kuwania ubingwa,"
"Bado naamini tulistahili kushinda kombe kama siyo kudhurumiwa baadhi ya michezo na marefa na TFF.
Sasa nafurahi timu imepata viongozi wapya nimewaambia wajipange kwa ajili ya msimu ujao"
"Hatutaki tena haya ya mwaka huu yatukute msimu ujao. Tunahitaji kuwa na timu imara itakayoshinda na kutwaa ubingwa mapema.
"Tutatengeneza timu imara, tutasajili wachezaji wa kiwango cha juu ambao watafanya timu yetu iwe kali".



0 Comments