


Kiungo wa Klabu ya Yanga Mcongomani, Pappy Kabamba Tshishimbi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Jangwani Jijini Dar es salaam.
Ikumbukwe mkataba wa Tshishimbi ulikuwa unafikia tamati msimu huu, Tshishimbi ni moja ya chaguo la mwalimu kama sehemu ya kuimarisha kikosi cha ushindi msimu ujao.
Tshishimbi amesaini mkataba huo mbele ya makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Ndg Fredrick Mwakalebela.



0 Comments