KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hana hesabu za kutwaa ubingwa msimu huu hivyo anawashukuru mashabiki kwa sapoti yao pamoja na wachezaji kupambana kupata matokeo.
Yanga ilikuwa na kete moja mkononi ya kuirudisha kwenye michuano ya kimataifa ambayo ilikuwa ni kombe la Shirikisho na kutolewa kwake na Lipuli kumepoteza matumaini ya kikosi hicho kukwea pipa msimu ujao kutokana na kasi ya wapinzani wao Simba kwenye ligi.
Zahera amesema aliwaambia wachezaji wake kwamba muda uliopo kwao ni kushika nafasi sita za juu na sio kuwa chini ya hapo ili wasishuke daraja msimu ujao.
"Niliwaambia wachezaji wangu kwamba tunaweza kupambana na kupata matokeo ila tushishuke ndani ya 10 bora afadhali tuwe nafasi ya sita na ya saba kuliko kuwa chini zaidi.
"Namshukuru Mungu mpaka sasa tumevuka lengo letu na tumeongoza ligi kwa muda mrefu tukiwa na pointi nyingi, hivyo kwa sasa inafaa kujipanga kwa ajili ya msimu ujao kuja na hesabu mpya na malengo mapya," amesema Zahera.
Yanga kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 80 baada ya kucheza michezo 34 na kinara ni Simba mwenye pointi 81 baada ya kucheza michezo 31.
0 Comments