

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa kikosi cha Yanga ni imara na kinauwezo wa kushindana na timu yoyote ndani na nje ya Tanzania kama ilivyo Simba.
Tambwe ambaye amecheza timu zote mbili kubwa za bongo, ambao ni Simba na Yanga mpaka sasa amepachika mabao 72 kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kutua bongo.
"Yanga ni timu imara na ina uwezo wa kushindana na timu nyingi hapa bongo na nje ya bongo, kwa kuwa tumecheza mechi nyingi za kimataifa hali inayotufanya tuwe imara kwenye ushindani.
"Kwa sasa ni suala la mpito tu ambalo tunalipitia ila bado wachezaji tunafanya vizuri hata ukitazama mpaka sasa tumepambana na tumejikusanyia pointi 80 kwenye ligi si haba, hata wapinzani wetu Simba nao wapo vizuri isipokuwa tunapishana vitu vidogo tu na ndio maana tunashindana nao," amesema Tambwe.




0 Comments