Asikwambie mtu kitu kuhusu usajili kuelekea Dirisha kubwa lijalo la Usajili kwani timu mbalimbali zimeendelea kutajwa kuwawania baadhi ya nyota ambao wamekuwa wakionekana kuwafaa katika timu zao.


Unakumbuka vyema lile sakata la Azam Fc kutaka kuongeza mkataba na aliyewahi kuwa nyota wa Yanga Obrey Chirwa lakini nyota huyo akachomoa na kuwaambia Azam Fc kusubiri mpaka mkataba wake wa sasa umalizike kwanza.

Sasa inaelezwa kuwa kumbe nyuma ya sakata hilo msomaji wa Kwata Unit kuna mkono wa Simba ambao inaelezwa walianza kumwania nyota huyo toka akiwa Yanga lakini ikashindikana na sasa inaweza ikawa rahisi kama watahitaji saini yake kwani atakuwa mchezaji huru.

Inaelezwa kuwa kama mambo yataenda sawa basi msimu ujao anaweza akavaa uzi mweupe na mwekundu kama mchezaji wa Simba.