KOCHA wa kikosi cha Singida United, Fred Minziro amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mchezo wake wa kesho dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa uwanja uwanja wa Namfua, Singida.
Minziro amesema anatambua ligi ni ngumu na kila timu inapambana kupata matokeo hivyo hatazembea kuonyesha ushindani.
"Tunahitaji pointi tatu, ligi kwa sasa imekuwa na ushindani ambapo kila timu inatafuta matokeo, muda wetu ni sasa kupata pointi tatu.
"Tutakuwa uwanja wa nyumbani na mashabiki watakuwa wetu, nina imani kupitia sapoti yao tutafanya vizuri," amesema Minziro.
Singida Unitd ipo nafasi ya saba imecheza michezo 35 imejikusanyia pointi 44.
0 Comments