

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimeondoka mkoani Morogoro kurudi jijini Dar es salaam ambapo timu hiyo itapokelewa Wilayani Kibaha na kulakiwa na mashabiki wake
Simba ilikabidhiwa ubingwa wa ligi kuu jana mkoani Morogoro baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Huu ni ubingwa wa pili mfululizo kwa Simba ambayo pia imefikisha mataji 20 ya ligi kuu ya Tanzania Bara
Shamrashamra za kusherehekea ubingwa huo zitaanzia Kibaha na matukio mbalimbali yataendelea kufanyika katika matawi ya Simba yaliyoko njiani kuelekea jijini Dar es salaam
Mapokezi makubwa yatakuwa Msimbazi jijini Dar es salaam, yalipo Makao Mkuu ya Simbacut
Tayari mashabiki wameanza kumiminika Kariakoo wakiwasubiri mashujaa wao waliomaliza kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 93
Msimu huu umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Simba kwani licha ya kutetea ubingwa wake, Simba ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Simba ni timu pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kufika hatua hiyo na kuisaidia Tanzania kuongezewa timu za kushiriki michuano ya CAF kuanzia msimu wa 2020/21
Timu nne zitashiriki michuano ya CAF msimu wa 2020/21



0 Comments