

Msafara wa kikosi cha Simba unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam leo saa sita mchana ukitokea mkoani Dodoma
Baada ya kutwaa ubingwa mkoani Singida jana, Simba ilielekea Dodoma ambapo wachezaji walipata mapumziko na leo asubuhi wataondoka kwa usafiri wa ndege kurejea Dar
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba, imewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwalaki mabingwa hao wa nchi
"Timu inayopendwa na Watanzania, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo leo saa 6:00 mchana itatua jijini Dar es Salaam. Wanasimba wote tukutane Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwapokea mashujaa wetu"



0 Comments