


Kikosi cha Simba kitacheza mchezo wa kufunga Ligi Kuu Bara leo Jumanne dhidi ya Mtibwa Sugar na mara baada ya kumalizika mabingwa hao wa ligi watakabiziwa kombe na zawadi zao za ubingwa.
Baada ya mchezo huo kikosi cha Simba kitaanza safari ya kurudi Dar es Salaam Jumatano watakapofika Kibaha wataanza shangwe na sherehe za ubingwa.
Kwa wachezaji, makocha na viongozi watakuwa wakisalimiana na mashabiki watakaokuwa wamejitokeza pembezoni mwa barabara.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara alisema mara baada ya kufika Kibaha nje ya kidogo ya Dar es Salaam tukiwa njiani tunatoka Morogoro ndio sherehe zitaanzia hapo kuwaonesha mashabiki wetu lile kombe.
“Sherehe zitakuwa za aina yake kwani tumepanga ratiba nzuri na kila mwanachama na shabiki wa Simba wasogee barabarani siku ya Jumatano kwani tutakuwa tunapita na shangwe la aina yake,” alisema
The post Simba Kuanza Shangwe la Ubingwa Leo – Video appeared first on Global Publishers.



0 Comments