Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Jimbo la Donge wamekataa kupitisha ripoti ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya Mbunge wa Jimbo hilo Sadifa Juma Khamis ya kipindi cha miaka mitatu kutoka 2015 hadi 2019, wakidai kuwa ripoti hiyo haina ukweli.
Wajumbe hao wamefikia maamuzi hayo baada ya Mbunge huyo kuiwasilisha kwao Kisha kutakiwa kuipigia kura,ambapo kura zilizoikataa ripoti hiyo kuwa 26 huku zilizoikubali zilikua 17 na kura 15 ziliharibika.
Licha ya Sadifa kuonekana kutumia muda mwingi wa zaid ya masaa matatu kwa ajili ya kuilezea na kuichambha ripoti hiyo,lakini haikufua dafu kutokana na wajumbe hao kudai kuwa anachokieleza ni cha kutunga tuu.
Baadhi ya wajumbe hao alisema alichokiandika na kukiweka wazi kwao hakina uhalisia na utekelezaji wa ilani ya CCM katika Jimbo hilo kutokana na ahadi alitoa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mmoja wa wajumbe hao,Juma Juma alisema hakuna wamechoka na uongo wa Mbunge hiyo ambaye hana mashirikiano mema na wananchi wake.
Alisema wanachi wana shida nyingi na kwa mujibu wa ilani ya CCM inamlazimu Mbunge hiyo kuteleza Yale aliyoyaahidi kwa wananchi, lakini hakuna ichofanya badaka yake ametoa ripoti ya uongo.
Thubeti Mzee Juma alisema miongoni mwa mambo ambayo Mbunge hiyo aliahidi ameshanunua tekreka mbili kwa ajili ya kilimo Jimboni humo,lakini Hadi leo hakuna hata trekta moja alikifikisha Jimboni humo.
“Tunachoshangaa Mbunge wetu huyu amekua akiahidi lakini hana anachotekeza,kitendo ambacho leo hii kimetuoa nguvu ya kukataa ripoti yake ambayo imejaa uongo” alisema.
Suleiman Haroun Jecha lisema mbali hilo lakini pia kwa upande wa eneo la Mahonda Mbunge huyo aliahidi kujenga ofisi ya Mbunge, ili kuondosha usumbufu wa wananchi kumtafuta kiongozi was huyo lakini hadi Leo hakuna alichotekeza.
“wananchi walipaga matumaini mazuri ya kuonana na kiongozi huyo baada ya kuabidi kujenga ofisi yake, lakini inatia aibu Hadi leo hii hakuna lolote alikifanya, Jambo ambali limewavunja moyo wananchi” alisema.
Alisema mbali ya hayo Mbunge huyo pia amekuwa mgumu kutekeleza shida za wananchi wake, likiwamo latizo la maji safi na salama,afya,uwezeshaji,kilimo na Mambo mengine mbali mbali ya kijamii.
Akitoa ufafanuzi wa tuhuma hizo pamoja ba kuelezea Mambo aliyotekeleza katika kipindi Cha mwaka 2015 Hadi 2019 Jimboni huyo,Sadifa alisema hakuna tatizo hata moja aliloliahidi Jimboni huyo Kish asitekeleze.
Alisema kilichotokea katika mkutano huo ni mambo ya kupangwa ili kuonekani hafanyi Jambo pamoja na kumtia doa baya kwa wananchi wake.
“Hili ni dhahiri kuwa ni tukio ambalo limepangwa leo hii wajumbe hao wanisimange na kunikatalia Mambo niliyofanya, ila mimi nasema sitachoka kutoa huduma Jimboni humo” alisema.
Alisema katika kipindi ch uongozi wake Jimboni humo ametekeleza Mambo mbali mbali ikiwamo kufikisha huduma za maji safi na salama, kusaidia vituo vya afya, kujenga Shule, kusaidia vikundi vya uwezeshaji, huduma za umeme,kujenga matawi la CCM ,pamoja na huduma nyengine mbali mbali za kijamii.
Sadifa alisema licha ya wajumbe hao kumataa kupitisha ripoti yake lakini hatasita kutoa kila aina ya ushirikiano na wananchi wa Jimbo hilo akiamini kwamba, anachofanya ni kwa mujibu wa ilani ya CCM.
Kwa upande wa Katibu wa CCM Mkoa wa kaskazini Unguja, Mula Othman Zubeir alisema kilichotokea katika mkutano huo si suala la kawaida,akidai kwamba wajumbe wana haki ya kuikubali au kuikataa ripoti ya Mbunge huyo.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu wa chama Mbunge huyo anapaswa kujipanga upya Kisha kurudi kwa wajumbe hao ili kuelezea uhakisiay wa Mambo aliyotekeleza Jimboni humo, akiahi uongozi wa Jimbo utasimamia kazi hiyo.
0 Comments