

Rayvanny amzawadia Gari S2Kizzy
Tarehe 9 May miaka kadhaa iliyopita alizaliwa moja ya maproducer wanaotamba sana Tanzania na Afrika mashariki kwasasa S2Kizzy.
Katika kuadhimisha siku hiyo moja ya ya wasanii ambao wamekuwa wakifanya naye kazi na kutengeneza naye nyimbo ambazo zimekuwa nyimbo pendwa Rayvanny amempa zawadi S2Kizzy.
Rayvanny ambaye alitangaza zawadi hiyo ya gari wakati ambao alitokea kama Saplaiz katika studio za wasafi Fm wakati S2Kizzy akifanya Interview kwenye kipindi cha Block 89
Alitumia muda huo kutangaza zawadi ya gari kwa S2Kizzy producer wa ngoma zake kama Pochi nene Original na Remix lakini pia Tetema ngoma inayofanya vizuri sana kwasasa.
Akizungumza baada ya kupewa zawadi hiyo S2Kizzy ambaye kwanza alilia kwa furaha baada ya zawadi hiyo alisema alilia kutokana na kutotegemea kilichotokea na kuahidi atakuwa ndugu yake maisha yote.
The post Rayvanny amzawadia Gari S2Kizzy appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.



0 Comments