Windows

Picha: Wawili wakimataifa wasaini miaka miwili Yanga



Hayawi hayawi sasa yamekuwa ndiyo moja ya msemo ambao huwa unatamkwa na watu wengi hasa baada ya kusubiri jambo kisha jambo hilo ambalo mwanzo huonekana kama haliwezekani kuwezekana.


Wakati wengi wakiamini Yanga haina hela na haiwezi kusajili mchezaji yoyote yule wa kiwango cha Juu Yanga imeanza kuwaonyesha kuwa wao wanaweza kusajili mchezaji wa kiwango cha Juu na wamejipanga kuhakikisha wanakuwa na kikosi bora msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Baada ya juzi na jana kukujuza kuhusu Yanga kumalizana na wachezaji Patrick Sibomana kutoka Rwanda anayekipiga Mukura Fc ya nchini humo na jana tukakujuza kuhusu mchezaji Issa Bigirimana anayecheza APR ya Rwanda basi mipango hiyo yote imekamilika kwa Yanga kuweza kumalizana nao.



Yanga msomaji wa Kwata Unit imefanikiwa kuwasaini wachezaji hao kwa kandarasi ya miaka miwili kila mmoja kucheza na kuvaa jezi za njano na kijani kwa misimu hiyo miwili.

Post a Comment

0 Comments