Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amerejea nchini leo sambamba na mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo
Zahera aliondoka na mshambuliaji huyo mapema wiki hii akiaga kwenda kushughulikia mambo binafsi
Hata hivyo imebainika Zahera aliambatana na Makambo hadi Guinea ambako walifanya mazungumzo na klabu ya Horoya AC
Baadae zilisambaa picha mitandaoni zikimuonyesha Makambo akisaini mkataba wa kuitumikia Horoya AC
Zahera amefafanua tukio hilo pamoja na tuhuma zinazotolewa juu yake kuwa wakala wa Makambocut
"Mimi sio wakala wa Makambo, niliambatana nae kwa kuwa aliomba niende nae," amesema
"Timu ya Horoya AC ilimuhitaji na ni kweli mazungumzo yamefanyika, kilichobaki ni wao kumalizana na Yanga"
"Makambo ni mchezaji halali wa Yanga, alisajiliwa akiwa mchezaji huru. Kama atauzwa, fedha zote za usajili wake italipwa Yanga"
"Makambo sio mshambuliaji pekee duniani, kama Horoya watamnunua, tutaleta mshambuliaji mwingine"
Aidha kuhusu Makambo kusaini mkataba wa miaka mitatu Horoya AC, Zahera ametaka maswali waulizwe Horoya Fc waliosambaza picha zinazomuonyesha akisaini lakini amesisitiza walichofanya ni mazungumzo ya awali
Hatma ya Makambo kutua Horoya AC iko mikononi mwa Yanga
K
0 Comments