

BAADA ya kupoteza mchezowake wa jana kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nswanzurimo amesema kuwa kinachoiponza Simba kupokea vichapo ikiwa nje kwenye mashindano ya kimataifa ni kubebwa na waamuzi ambao wanashindwa kutafsri sheria 17.
Nswanzurimo amesema kuwa hajaona uwezo wa kikosi cha Simba jana kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya, kwani kwa kiasi kikubwa walitawala mpira mwanzo mwisho ila waamuzi wakawaponza.
"Unajua timu kubwa kama Simba imetoka kuwakilisha nchi michuano ya kimataifa, waamuzi wa hapa wanaibeba sana sasa wakitoka nje huko wanapokea vichapo kwa kuwa hakuna anayewajua, ili kuboresha ligi tunahitaji kumpata mshindi bora na halali na sio mshindi wa kuchaguliwa.
"Nimeumia sana kupoteza mchezo wangu ilihali nilistahili kushinda hii sio sawa siwezi kuwalaumu waamuzi moja kwa moja ila wanachangia kudumaza maendeleo ya mpira wetu, kuna umuhimu wa kufuata sheria na utaratibu ili kukuza soka letu," amesema.
Simba kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika haikushinda mchezo hata mmoja nje iliishia kupewa zigo la mabao na timu ya As Vita mabao 5-0, Al Ahly mabao 5-0 na JS Saoura mabao 2-0.



0 Comments