

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kwa sasa wachezaji wake wamechoka kutokana na kushindwa kupata muda wa kupumzika baada ya kucheza michezo mingi kwa wakati mmoja kwenye ligi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa amecheza michezo 10 ndani ya siku 24 hali ambayo imefanya wachezaji wake wachoke.
"Unajua tumecheza mechi 10 ndani ya siku 24 tu, hili jambo sio jepesi na wachezaji wangu wanachoka wanashindwa kupata muda wa kupumzika, ratiba imewabana wanashindwa kupata muda wa kurejea kwenye ubora wao.
"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri licha ya kupoteza kwenye mechi zetu zote mbili nje na ndani ni jambo la kawaida kwa kuwa huu ni mpira na kitu chochote kinaweza kutokea, mashabiki waendelee kutupa sapoti kuna jambo jema linakuja kwa ajili yao," amesema.
Simba imeshindwa kufurukuta msimu huu mbele ya Kagera Sugar baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Kaitaba kufungwa mabao 2-1 na mchezo wa jana kufungwa bao 1-0.




0 Comments