Marekani inapeleka kundi la manowari za kivita zinazobeba ndege za kivita katika eneo la mashariki ya kati kabla ya muda uliopangwa na kuonya kwamba Iran na jeshi lake zinaonesha hali ya mbaya ya kuongezeka kwa ishara za uwezekano wa shambulio dhidi ya majeshi ya Marekani katika eneo hilo.
Kile kinachosababisha hatua hiyo bado hakijajulikana, lakini kinaonesha hali ya kuongezeka kwa wasi wasi kati ya utawala wa rais Donald Trump na taifa hilo la Kiislamu.
Mshauri wa usalama wa taifa John Bolton amesema Jumapili usiku kwamba Marekani inapeleka meli ya kivita ya USS Abraham Lincoln pamoja na kikosi cha mashambulizi kwenda katika eneo la mashariki ya kati, hatua inayokusudiwa kutoa ujumbe kwamba nguvu kubwa itatumika dhidi ya shambulio lolote dhidi ya vikosi vya jeshi la Marekani ama washirika wake.
Bolton ameongeza kwamba Marekani haitafuti kupiga vita na utawala wa Iran, lakini majeshi ya nchi hiyo yamejitayarisha kujibu shambulio lolote.
0 Comments