Manchester City imefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuilaza Brighton mabao 4-1
Aidha Liverpool nayo imefanikiwa kushinda mabao 2-0 dhidi ya Wolves lakini wameshindwa kuipiku Man City iliyotwaa ubingwa baada ya kufikisha alama 98
Kwa mara nyingine Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amedhihirisha umwamba wake kwenye ligi hiyo kwa kutwaa ubingwa mara mbili akiwa ndio kwanza ameingia msimu wa tatu
Ligi Kuu ya Uingereza imefika tamati leo ambapo mabingwa hao wateule wamekabidhiwa taji lao
Washambuliaji Mo Salah, Sadio Mane na Pierre Emerick Aubameyang wameibuka kuwa wafungaji bora wa ligi hiyo wote wakifunga mabao 22
Alison Becker, mlinda lango wa Liverpool ameibuka kuwa kipa bora wa ligi hiyo

0 Comments