Windows

Magid Mjengwa amkumbukavyo Dkt,Reginald Mengi

Mzee Mengi ameagwa jana pale ukumbi wa Karemjee jijini Dar es Salam, nasikitika sikuweza kuwa mmoja wa waliofika kumuaga marehemu huyo kipenzi cha wengi.

Nitamkumbuka Mzee Mengi kama wanavomkumbuka wengine,nilipata  bahati ya kukutana na kuzungumza nae. Kuna mengi nilijifunza kutoka kwake kwa muda mrefu.

Mwaka 2008 nikiwa namiliki jarida la Kwanza Jamii lilikuwa likitoa habari zaidi kwa ajili ya jamii ya watu wa vijijini nwa kwa vile lengo lilikua ni kupenda   jarida hilo lifahamike na jamii kupitia kusomwa kwenye kipindi cha magazeti ITV.

Rafiki yangu Martha Kente alifahamiana na Regina Mengi. Aliniunganisha na Regina na nilikutana na Regina na kNamkumbuka kuwa alikuwa dada mwema na mwenye akili na busara nyingi. Alinisikiliza kwa makini.Kuna aliyonishauri pia ili kufanikisha kuimarisha jarida lile la kijamii. Jarida lilisomwa ITV.

Ikafika siku pia Regina akanipigia simu kunieleza kuwa Mzee angependa kukutana nami basi asubuhi moja nilifika pale Haidary Plaza, ilipokuwa ofisi ya Mzee Mengi. Joyce Mhavile alinipokea. Nilikaribishwa ofisini kwa Mzee Mengi alikua mtu mcheshi na mchangamfu wa aina yake.

Tukiwa wawili, Mzee Mengi na mimi, tulikaa kwenye kona ya ofisi yake na kuzungumza kwa kirefu juu ya masuala ya media na mwenendo wa nchi yetu kwa ujumla kwa hakika siku hili ilikua faraja kubwa sana kwani nilijifunza vitu vingi mno.

Mara ya pili kukutana na Mzee Mengi ilikuwa ni pale Ukumbi wa Makumbusho. Ni kwenye siku ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Sweden na Tanzania. Tulisalimiana tu ( Juu pichani) na hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya mwisho kuonana ana kwa ana na Mzee wetu Mengi.

Nachukua fursa hii kumpa pole nyingi dada yangu Regina Mengi. Niko pamoja nae, mke mpenzi wa Mzee Mengi, na familia yao katika wakati huu mgumu kwao.


Post a Comment

0 Comments