Windows

Kabla Zahera hajaondoka, Yanga kusajili wachezaji nane wiki hii


Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo May 29 2019 kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya Taifa ya nchi hiyo, yeye akiwa kocha Msaidizi

Yanga itacheza na Azam Fc May 28 mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu na baada ya mchezo huo Zahera ataondoka usiku

Zahera amesema DR Congo inakwenda kuweka kambi Hispania kujiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika Misri kuanzia Juni 21 2019

Mcongoman huyo amefichua kuwa kabla ya kuondoka atakamilisha usajili wa nyota saba au nanecut

"Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kutengeneza timu yetu kwa ajili ya msimu ujao. Tunafanya mazungumzo na wachezaji wengi," amesema Zahera

"Mimi nasafiri tarehe 29, tunacheza mechi ya Azam na usiku uleule saa nane mimi nakamata ndege. Sisi tunaenda Hispania tarehe 31 tunaingia kambini na timu ya Taifa"

"Kabla ya mimi kusafiri nadhani itakuwa karibu wachezaji saba, nane watakuwa wamesaini kwa timu yetu ya Yanga"

Zahera ameongeza kuwa usajili wa timu yake unalenga kukiimarisha kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao

Anaamini wachezaji hao watakaosajiliwa wataingozea Yanga makali msimu ujao

Post a Comment

0 Comments