Windows

FAIDA ZA KUFUNGA RAMADHANI KWA WACHEZAJI



Katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, kuna wachezaji ambao wamefunga. Dr. Sylvester Safi daktari wa Singida United amezungumzia afya za wachezaji wanaofunga na kutoa ushauri wa vyakula wanavyopaswa kula katika kipindi hiki.
.
Kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, baadhi ya wachezaji wamefunga ninachoweza kusema faida ni nyingi kuliko hasara za kufunga.
.
Kuna kitu tunaita transformation ya sukari ambayo tayari imehifadhiwa mwilini kutoka sehemu mbalimbali za mwili, inabadilishwa kutumika wakati wa ziada ambapo sukari inakuwa haipo mwilini.
.
Kinachotokea kwa wachezaji wetu na madhara wanayoweza kupata wakati wa mfungo wakiwa uwanjani wanacheza ni kukosa glucose.
.
Lakini tunawaelekeza sana watumie vyakula ambavyo vina carbohydrate kwa maana ya wanga mwingi halafu wapate maji mengi ambayo yatasaidia mmeng'enyo wa chakula lakini system zote za mwili zinahitaji maji ili ziweze kufanyakazi vizuri.
.
Tunashauri pia wapate vyakula vyenye vitamins kwa ajili ya ku-strengthen misuli. Kikubwa zaidi baada ya mazoezi tunawashauri wapate chakula laini kama uji ili kulainisha mmeng'enyo wa chakula halafu badae wapate vyakula vyenye vitu nilivyovitaja.
.
Faida ya kufunga kwa wachezaji
.
Kunasaidia mmeng'enyo wa chakula, kunasaidia kuepukana na magonjwa mbalimbali kama strock [kiharusi].
.
Kufunga kunasaidia kupunguza mafuta ambayo yanagandiana kwenye mzunguko wa damu (kwenye misuli inayotumika kusambaza damu). Mafuta hayo yanapopungua mchezaji anakua kwenye hali nzuri ya kuepuka kupata magonjwa yatokanayo na matatizo ya kuwa na mafuta mengi.
.
Kingine mchezaji anapungua uzito [sio sana] lakini anaepuka diabetes na vitu vingine.

Kwa hiyo mchezaji ambaye anafunga anapata faida nyingi ukilinganisha na yule ambaye hajafunga. Tunawashauri wachezaji waliofunga, wanapomaliza mazoezi au mechi, wapate maji na kupumzika na kupata vyakula nilivyoviorodhesha.

RAMADHAN KAREEM🌙

Post a Comment

0 Comments