TURIN, Italia
DIDIER Deschamps ameibuka mstari wa mbele katika orodha ya makocha wanaotakiwa kwenda kukalia kiti cha Massimiliano Allegri pale Juventus.
Deschamps licha ya kuichezea, pia aliwahi kuinoa Juve, akibeba mara mbili mfululizo taji la Serie A.
Ni miezi michache tu imepita tangu Deschamps mwenye umri wa miaka 50 alipoipa Ufaransa ubingwa wa Kombe la Dunia.
Curry aongoza mauaji Warriors
LOS ANGELES, Marekani
MKALI Stephen Curry juzi alikuwa kwenye kiwango cha juu wakati timu yake ya Golden State Warriors ikiichabanga Portland Trail Blazers, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Kikapu (NBA).
Warriors walishinda pointi 116-94, Curry akifunga 36 ikiwamo kufunga mara tisa kwa mtindo wa pointi tatu.
Ukiwa ni mchezo wa kwanza, leo mabingwa watetezi hao wa NBA watakuwa nyumbani kurudiana na Trail Blazers.
Hapana chezea Moses huko Uturuki
ANAKARA, Uturuki
STAA wa Chelsea anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce, ametajwa kuwa ndiye mchezaji wa bei mbaya zaidi Ligi Kuu ya Uturuki.
Moses mwenye thamani ya euro milioni 20, amewapiku wakali wengine kama Adem Ljajic, Badou Ndiaye, Edin Visca, Yusuf Yazici na Henry Onyekuru.
Mkali huyo, Moses, anacheza kwa mkopo Fenerbahce akitokea Chelsea ya Magharibi mwa Jiji la London.
Beki Inter: Hao Napoli hawatuambii kitu
MILAN, Italia
NYOTA wa Inter Milan raia wa Ghana, Kwadwo Asamoah, anaamini wataipiku Napoli katika kuiwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Huku wao wakiwa nafasi ya tatu, Inter watatakiwa kuzichukua pointi tatu za Napoli wanaoshika nafasi ya pili, mchezo utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii.
Inter waliyaweka hai matumaini yao kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chievo katika mtanange wa Jumatatu.
Fletcher kupewa ubosi Old Trafford
MANCHESTER, England
Kuelekea maandalizi ya msimu ujao, Manchester United wanataka kuajiri mkurugenzi wa ufundi na ni nyota wao wa zamani, Darren Fletcher, ndiye anayepewa nafasi kubwa.
Fletcher mwenye umri wa miaka 35, alicheza zaidi ya mechi 300 akiwa na uzi wa Mashetani Wekundu lakini aliondoka mwaka 2015.
Wakati huo huo, Rio Ferdinand na Edwin van der Sar nao wanahusishwa na kibarua hicho.Mkataba wake wa sasa Gundogan utafikia tamati majira ya kiangazi hapo mwakani na msisitizo wake ni kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Kocha Ajax: Barca mtanisubiri sana
AMSTERDAM, Uholanzi
HUKU Barcelona wakihaha kumsaka, kocha wa Ajax, Erik ten Hag, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuwaacha vijana wake hao walioitikisa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kwa kufika nusu fainali.
Kwa muda sasa, zimekuwapo taarifa kuwa mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 49, anatakiwa kwenda kukalia kiti cha Ernesto Valverde.
Ieleweke kuwa mbali ya Barca, Chelsea na Bayern Munich nazo zinamtaka lakini Mholanzi huyo amesema hana mpango na ofa zao.
Sikia hii ya PSG kwa Madrid
MADRID, Hispania
MATAJIRI wa PSG wamevunja kibubu unaambiwa, chanzo kikiwa ni majembe matatu wanayotaka kuyachukua ndani ya kikosi cha Real Madrid.
Kwa mujibu wa taarifa ya kituo cha runinga cha Fox Sports, PSG imepanga kukitumia kipindi hiki cha usajili wa kiangazi kutekeleza mpango wao huo.
Nyota hao ni Gareth Bale, Isco na Toni Kroos, ikielezwa kuwa wote wameandaliwa euro milioni 210.
Sanchez akataliwa Arsenal
LONDON, England
MKONGWE wa Arsenal, Ray Parlour, amedai kuwa Alexis Sanchez amekwisha, hivyo hawezi kupata nafasi ya kurejea klabuni hapo hata kwa bahati mbaya.
Sanchez mwenye umri wa miaka 30, aliumaliza vibaya msimu huu, akiwa na mabao mawili tu katika mechi 27 za Ligi Kuu ya England.
“Alikuwa mzuri sana pale Arsenal. Sina uhakika kama mashabiki watamkubali,” alisema Parlour na kuongeza: “Amekwisha kweli…”
0 Comments