![](https://4.bp.blogspot.com/-oWBF5rnYXzE/W7uedCj85EI/AAAAAAAAJdY/0jTfLk_9khU5DTaZ6o-KfH_A3hrpI_ZJQCLcBGAs/s320/aaaaaaaaaa.jpg)
![](https://1.bp.blogspot.com/-5UdUkBxLqPE/W7ujeNJL4XI/AAAAAAAAJds/dBugYDvLQq0WptS1YBXQGjJB_vJFBWL7wCLcBGAs/s320/yyyyyyyyyyyy.jpg)
Mkurugenzi wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema baada ya kufanya mazungumzo na Chirwa na kutofikia mwafaka walisitisha na kuangalia mwisho wa msimu kama wataenda sawa kwa vile akili zao kwa sasa zipo kwenye fainali ya Kombe la FA.
“Tulianza kuzungumza naye, ila baada ya kuona mambo hayaendi tukaacha jambo hilo ili tufanye mengine kwa kwa ufasaha,” alisema.
Mbali na hilo, aliweka sawa kwa kile kinachozungumzwa na wadau wa soka nchini kwamba Azam ina kila kitu, jambo alilolipinga akidai sio kweli kwa namna Simba na Yanga wanavyowalipa wachezaji wao wenyewe hawawezi kufikia gharama hizo.
“Ni kweli tuna uwanja, gym lakini hata Simba na Yanga zinafanya mazoezi ya gym, halafu wao ndio wanaowalipa dau kubwa wachezaji wao kuanzia pesa za usajili hadi mishahara yao, jambo ambalo Azam FC, hatuna uwezo nalo.

0 Comments