Uongozi wa klabu ya Bandari Fc inayoshiriki ligi kuu ya Kenya umedai kuwa mlinda lango wake Farouq Shikalo bado ana mkataba wa muda mrefu na hawako tayari kumuuza msimu huu
Shikalo alikaribia kusajiliwa na Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo uliofungwa Disemba 15 2018 kabla ya usajili wake kukwama dakika za majeruhi tukio lililomkera kocha Mwinyi Zahera na kuishushia lawama Kamati ya usajili iliyokuwa chini ya Hussein Nyika
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bandari FC Edward Oduor amesema mlinda lango huyo ana mkataba wa miaka miwili na Bandari Fc
Baada ya kuachana na Beno Kakolanya, Yanga inatarajiwa kusajili mlinda lango mwingine wa kuchukua nafasi yake
Aidha kumekuwa na mapendekezo kuwa mabingwa hao wa kihistoria wanapaswa kusaka walinda lango wawili wenye uwezo wa juu ambao wataisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa msimu ujao
Mabadiliko makubwa ya kikosi cha Yanga yanatarajiwa msimu huu

0 Comments