Windows

ZAHERA: TUMEIBIWA POINTI 10 LIGI KUU


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amelalamika kuwa wameibiwa pointi 10 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kocha huyo amefunguka kwa kusema "Ligi hii sisi tutaicheza nguvu mpaka mwisho tukimaliza tutaangalia hata kama haya mambo yanayotokea.

"Tukimaliza tutaangalia wapi walitufanyia mambo ya hovyo, ligi tutacheza mpaka mechi ya mwisho na tutacheza na hamu yetu ya kuwina kila mechi.

Tukimaliza tutafanya hesabu tutaangalia wapi tulifanyie nani wapi walitufanyia vitu ya hovyo.

"Hapa leo nimeisha angalia karibu pointi kumi wametuibia.

"Mimi naita kutuibia eeh , najua wanatuibia kabisa zipo mechi karibu nne wametuibia mapointi kabisa .

"Mimi najua kabisa mpango unafanyika , sisi hatushindwi uwanjani tunashindwa vile mipango ambayo wanatufanyia, hatuchezi na timu moja tunajua tunacheza na timu nyingi." amesema Zahera.

CHANZO: UHURU FM

Post a Comment

0 Comments