Windows

SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA KUBANWA MBAVU NA WANA 'BOLINGO' SASA WAJA NA SERA MPYA NGUMU KINOMA


UONGOZI wa Simba umetoa tamko baada ya kubanwa mbavu na TP Mazembe kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Simba leo wamelazimisha sare kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya robo fainali wakiwa nyumbani mbele ya TP Mazembe kwa kutoka suluhu bila kufungana.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ujumbe uliosomeka namna hii:-

"Alhamdulillah,jitihada hazizidi kudra ila tuendelee kushikamana ktk Dakika tisini za Jasho na Damu kule Congo!!," amesema Manara.

Simba watarudiana na TP Mazembe ugenini ambapo ili apenye sasa anatakiwa akashinde ugenini akipigwa safari inaishia Congo, ngoma ikiwa droo mshindi anatafutwa kwa njia ya penalti.

Post a Comment

0 Comments