

KIKOSI cha Simba jana kililazimisha suluhu ya kutofungana mbele ya TP Mazembe kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa nahodha wa Simba, John Bocco alipaisha mawinguni penalti dakika ya 59 baada ya mchezaji wa TP Mazembe kunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa mchezaji kukosa penalti ni kitu cha kawaida hivyo wanaomlaumu wanapaswa watambue mchango wa Bocco ndani ya Simba.
"Atakaemlaumu Bocco kukosa Penati, ni ugeni katika mpira kwa baadhi yetu, Bocco huyu huyu ndio anafunga Penati zote za Simba kila tunapopata, Bocco huyu huyu ndio alifunga Penati muhimu kule kitwe tulipocheza na Nkana.
"Penati ni pigo la bahati na huwa haina mwenyewe, ikiwa Messi mwenye mpira wake hukosa,Captain Bocco ni nani asikose? Ikumbukwe huyu kakosa na Mazembe,kuna mtu juzi tu kakosa na Ndanda.
"Tuwape nguvu wachezaji wetu ili wakapambane kule Lubumbashi,tuache lawama za hovyo hovyo," amesema Manara.




0 Comments