

Yanga imeshindwa kupata matokeo mazuri katika mechi mbili mfululizo baada ya kubanwa na Lipuli kule Iringa sasa Ndanda imefanikiwa kuchukua alama mbili katika mechi mbili za Yanga msimu huu.
Yanga ambayo ni kinara kwenye msimamo wa TPL imeshindwa kutamba mbele ya Ndanda, uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Matokeo hayo yamekuwa ya kiitoa kwenye reli Yanga katika kampeni ya ubingwa ambapo sasa itahitaji kuiombea Simba kupoteza zaidi ya michezo mitano ili kuweza kuchuana vyema kwenye mbio za TPL. Yanga imefikisha alama 68, Azam 62 na Simba 57 huku kukiwa na tofauti kubwa ya tofauti ya michezo kati ya Yanga/Azam na Simba.
Kwa mahesabu ya kawaida unaweza kuona Yanga imeanza kujitoa kwenye reli huku Simba ikionekana kunufaika na ubora wa kikosi.
Maoni: Sababu ya kutoka kwenye njia ya reli.
Upana wa kikosi.
Yanga kwa asilimia kubwa kikosi kinachoanza kwenye kila mchezo wa mashindano, zaidi ya wachezaji 6 mpaka 7 ni wale wale. Hiki kinapelekea kuchoka kwa wachezaji, tazama Yondani, Feisal Salum, Mrisho Ngassa tofauti na wapinzani wao Simba.
Mwalimu
Mwinyi Zahera ni kocha bora mpaka sasa kwa jinsi alivyokifanya kikosi cha Yanga kuwa tishio licha ya kuwa na kikosi finyu chenye wachezaji wengi wa kawaida. Mbali na ubora wake safari ya Congo imekuwa ikiwaacha Yanga kupoteza umakini wao tazama dhidi ya Lipuli.
Majeruhi.
Ibrahim Ajib ni mchezaji bora kwenye kikosi cha Yanga mpaka sasa akiwa na assist 13. Kukosekana kwake kumefanya, mzalishaji wa mabao kukosekana pia, Makambo kupotea, Tambwe kapotea nguvu za Paul Godfrey zikaishia sakafuni mithili ya kumwaga maji ambayo kawaida huwa hayazoleki. Yote haya yamepelekea Yanga kuwa katika wakati mgumu wa kutwaa ubingwa wa TPL hasa ukitazama inavyopata matokeo yake kama bahati tofauti na wapinzani wake wa karibu.



0 Comments