

Kikosi cha TP Mazembe kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kimewasili kikitokea Congo kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa Ndege maalum ya timu hiyo na baadae kuunganisha safari ya Dar es Salaam.
Ujio wa Mazembe umekuwa wa tahadhari kubwa ambayo imekuwa ikitafsiriwa tofauti na kila mmoja. Kikubwa unachoweza kukizungumza ni hofu juu yao. Wanakumbuka yaliyowakuta Al Ahly, AS Vital na pengine JS Soura wanaingia kiwewe.
Walipofika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam walikataa kutumia gari ambalo kwa kawaida huandaliwa na timu mwenyeji (Simba) badala yake wakatumia gari aina ya Coastal, unaweza kupata picha kitu kilicho akilini mwao. Ingawa kwa ujumla wake ndio soka la Afrika lilivyo.
Kimchezo TP Mazembe na Simba sio timu ngeni, kila mmoja anamjua mpinzani wake vizuri tangu mwaka 2011 ingawa Tout Puissant wanarekodi jadidi kwa Simba, wakiwa mabingwa mara 5 wa michuano ya Ligi ya Mabingwa.
KIKOSI.
Simba inajivunia kikosi kilicho na muunganiko bora. Simba pia ina kikosi ambacho kina mchanganyiko wa damu changa Mzamiru Yasni, Rashid Juma, Jonas Mkude pamoja na wakongwe kama John Bocco, Emmanuel Okwi, Erasto Nyoni wakati TP ikiwa na wachezaji wenye wastani wa umri mkubwa.
UZOEFU.
Simba haina uzoefu wa kutosha kulinganisha na TP Mazembe ambao wastani kila mmoja ameonja utamu wa kubeba taji kubwa kwa ngazi ya vilabu, tofauti na Simba ambayo baadhi ya wachezaji ndio wamecheza michuano hiyo kwa mda sasa kama Meddie Kagere na Okwi.
Mazembe watamenyana na Simba Uwanja wa Taifa kesho Jumamosi ya April 6, 2019 huku kauli mbiu ya Simba ikiwa ni Yes We Can.



0 Comments