

Winga wa timu ya Yanga, Deus Kaseke, amesema kuwa walistahili kushinda mchezo wao wa juzi dhidi ya Ndanda.
Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 kwenye Uwanaja wa Nangwanda Sijaona katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa mjini Mtwara.
Kutokana na matokeo kuwa hivyo, Kaseke amesema walijitahidi kucheza mpira na walimiliki kwa asilimia nyingi lakini bahati haikuwa yao.
Amefunguka kuwa Ndanda walikuwa kama na bahati na akisema matokeo huwa yanakuwa ya aina tatu ikiwemo ni kushinda, sare na kufungwa.
Mbali na kutoa sare, Kaseke anaamini kuwa sare hiyo itasababisha kuzidi kupunguza nguvu za kupigania ubingwa ambao unawaniwa pia na watani zao wa jadi, Simba.




0 Comments