Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, ameandaa dozi nene kwa ajili ya wapinzani wao TP Mazembe kuhakikisha wanafanikiwa kuwafunga katika uwanja wa nyumbani.
Kagere amesema atahakikisha anapiga tizi la maana kuelekea mchezo huo. Simba inatarajia kuikaribisha Mazembe Aprili 6 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Kagere ni mmoja wa vinara wa ufungaji kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, akiwa na mabao sita katika michuano hiyo huku akiwa ameifungia timu hiyo mabao 13 kwenye ligi.
Kagere amesema kuwa, ili kuweza kufanikiwa kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Mazembe, ni kuhakikisha anafanya mazoezi ya nguvu kuelekea mchezo huo ili kufanya vizuri.
“Mechi yetu na TP Mazembe itakuwa ngumu na ushindani mkubwa, kikubwa ni kufanya mazoezi sana ili tufanikiwe kufanya vyema katika mchezo huo,” alisema Kagere.
Kwa sasa uongozi wa Klabu ya Simba, upo katika mchakato wa kuandaa mazingira ya mchezo huo ili kujua watawakabili vipi wapinzani wao kutokana na vikao vya mara kwa mara wanavyokaa, ikiwemo suala zima la uhamasishaji.
0 Comments