YANGA wamesema watawafikiria waliokuwa wagombea wa klabu hiyo, Jonas Thiboroha na Baraka
Igangula pamoja na wajumbe wengine ambao walichukua fomu kwenye uchaguzi uliovunjika Januari 13.
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay aliliambia Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili kwamba
wagombea waliochukua fomu huko nyuma suala lao litafikishwa katika kamati husika.
“Mchakato wa uchaguzi unaendelea, utapangwa baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura lakini siwezi kujua lini utaitishwa ili kujua tarehe ya uchaguzi.
“Wagombea wa mwanzo ambao walichukua fomu katika uchaguzi uliovunjika watafikiriwa na kamati husika kuona tutafanya nini,” alisema Lukumay.
Wagombea ambao walichukua fomu katika uchaguzi uliovunjika ni pamoja na Tiboroha, Igangula na kwa upande wa Makamu Mwenyekiti alikuwepo, Yono Kivela, Pindu Luhoyo, Salum Magege Chotta na Titus Osoro.
0 Comments