Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza kumshitaki staa wa Brazil na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar kwa kosa la kuandika maneno ya kichochezi kuhusu muamuzi wa mchezo wao wa UEFA Champions League dhidi ya Man United uliyomalizika kwa Man United kupata goli la penati dakika za majeruhi katika ushindi wa 3-1 na kuitoa PSG.
Neymar hakuwa sehemu ya mchezo huo kwa sababu ya kuwa majeruhi lakini alikuwa akiufuatilia mwanzo mwisho kutokana na timu yake ila penati iliyotolewa na muamuzi dakika za majeruhi ilimfanya aandike maneno ya jazba kupitia ukurasa wake wa instagram ambayo yalikuwa yanaashiria kuwa Man United imebebwa.
“Hata kama wakichukua watu wanne ambao hawajui mpira na wafutilie kwa picha za marudio za video taratibu, sio kweli (penati) ni namna gani (Kimpembe) alitumia mkono wake kwa nyuma kwa kuufuata mpira”>>>>Neymar Via Instagram
Goli la mwisho lililowapeleka hatua ya robo fainali Man United ndio lilizua gumzo lililopatikana kwam penati iliyopigwa na Marcus Rashford sekunde chache kabla ya game kuisha kwa madai ya Kimpembe wa PSG alishika mpira katika eneo la 18, baada ya kutolewa Neymar ambaye anakosekana kwa kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi, amelaumu na kueleza kuwa ile haikuwa penati.
0 Comments