IKIWA ni siku tisa tangu kituo cha Utangazaji cha Clouds Media kupata pigo kwa kuondokewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa kituo Ruge Mutahaba, chombo hicho cha habari kimepata pigo jingine tena leo kwa kuondokewa na mtangazaji Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya leo, Alhamisi, Machi 7, 2019.
Kupitia Ukurasa wa Istagram wa Clouds wameandika:“Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa Mkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #Ruge Mutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Mtangazaji wetu Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7, 2019).
“Tunamtukuza Mungu kwa maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.
Imeelezwa kuwa, Kibonde amefariki akiwa Mwanza na alianza kusumbuliwa na presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Ruge.Julai 10, 2018 mkewe Sara Kibonde alitangulia mbele za haki wakati akipatiwa matibabu hospital ya Hindu Mandal.
PUMZIKA KWA AMANI KIBONDE
0 Comments