UKISIKIA watu wanasema ametoa kali, basi lazima tukio liwe la kushangaza. Hebu sikia, msanii wa filamu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alivyofanya alipokutana na mwanamitindo Miriam Odemba na kutaka kupiga naye picha.
Kwanza alijitathimini, akagundua yeye ni mfupi kinoma kwa Odemba, akaona isiwe shida; kisa cha kupiga picha na kuonekana Andunje nini? Akaamua kuvuta kiti na kupanda juu yake ili walingane urefu.
Nadhani sharti alilopewa mpigapicha ni kutofikisha taswira miguu ili jamaa asije kuumbuka, unajua baadaye Steve Nyerere alisemaje?
“Nimeamua kujiongeza na kutumia akili ya kuzaliwa ili niweze kulingana na Miriam, ningesema nipige picha bila kupanda kwenye kiti ingekuwa kama ile picha ambayo niliwahi kupiga na Idris Sultan nikajikuta nimefika usawa wa kiuno chake.”
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar ambapo Steve Nyerere na Odemba walikutana katika kumjulia mtoto Hamisi anayesumbuliwa na tatizo la miguu
0 Comments