Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Anthony Martial amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kupata majeraha katika mchezo wa FA dhidi ya Wolverhampton Wanderers.
Straika huyo alicheza dakika zote 90 akiwa sehemu ya kipigo cha 2-1 mikononi mwa vijana wa kocha Nuno Espirito Santos ingawa alipata maumivu kidogo ya kifundo cha mguu.
Unaweza kusema mbuzi wa masikini hazai kutokana na hiki kilichompata Martial. Anthony Martial amerejea katika mchezo mmoja tu na kupata maumivu hayo akiwa amekaa nje kwa mwezi mmoja, tangu alipoumia kwenye mchezo dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG).
Ilikuwa mara ya kwanza baada ya mda mrefu kutoitwa kwenye kikosi cha Ufaransa lakini hivi sasa kocha Didier Deschamps ameamua kufanya mabadiliko madogo kwenye nafasi hiyo na kumuita Lemar Thomas kuwa sehemu yake.
Matabibu wa timu zote mbili Manchester United na Ufaransa wamekubaliana mchezaji huyo asalie kwenye mji wa Carrington kwa ajili ya matibabu zaidi. Kocha Ole Gunner Solskjaer anatumainia winga wake atarejea mda sio mrefu au kabla ya mchezo dhidi ya Watford mwishoni mwa mwezi wa tatu.
0 Comments