MWENYEKITI wa Kamati ya Uhamasishaji kuelekea mchezo wa ya Taifa Stars kufuzu michuano ya AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameshukuru mwitikio wa Watanzania ambao wamekuwa wakiisapoti timu hiyo na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuishabikia ili ishinde na kutinga michuano hiyo.
Amesema hayo leo Alhamisi, Machi 21, 2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, na kuwashukuru watu wote wanaotoa tiketi za bure kwa Watanzania kwenda uwanjani kuishangilia Taifa Stars Jumapili ijayo.
“Ninatoa ruhusa kwa daladala yoyote kutoka sehemu yoyote ya jiji la Dar, siku hiyo waendeshe route (njia) ya kutoka popote walipo kwenda Uwanja wa Taifa. Ukipata shida yoyote njiani nitafute mimi. Tukishinda mechi hii nitakahikikisha tunafanya party (karamu) kubwa sana ndani ya hili jiji la Dar na Tanzania kwa jumla.
“Leo asubuhi nimeongea na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na amekubali kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo. Kazi yangu kama mwenyekiti wa kamati hii ni kuiweka timu mikononi mwa Watanzania. Nashukuru media (vyombo vya habari) zote kwa kutuunga mkono kazi yetu. Ninaamini timu hii ipo mikononi mwa Tanzania rasmi. Twendeni uwanjani,” amesema Makonda.
0 Comments