Windows

LIVE: STAND UNITED 0- 0 SIMBA


MCHEZO  wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Stand United unaendelea Uwanja wa Kambarage ikiwa ni kipindi cha kwanza.

Mashabiki waliojitekeza leo ni wengi kuona namna ushindani ulivyo wa wababe hawa wa ligi dhidi ya Chama la wana.

Mpaka sasa hakuna timu iliyoona lango la mpinzani wake huku kikosi cha Stand United kikiwa imara kushambulia lango la Aishi Manula.

Asante Kwasi wa Simba alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 11 baada ya kumvuta jezi mchezaji wa Stand United.

Stand United wamepiga kona mbili mpaka sasa huku Simba wakiwa wamepiga kona moja mpaka sasa bila kuzaa matunda.

Post a Comment

0 Comments