Windows

Klopp adai hasajili tena hapo Liverpool



Liverpool imekuwa ikitajwa kuwinda huduma ya kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez sambamba na mchezaji Steven Bergwijn.ADVERTISEMENT



Liverpool, England. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kwamba wababe hao wa Anfield hawatahangaika kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.


Liverpool walifanya usajili mkubwa sana mwaka jana wakati ilipovunja rekodi za dunia kwenye uhamisho iliponasa Virgil van Dijk na Alisson Becker huku mastaa wengine iliyowanasa ni Naby Keita, Fabinho na Xherdan Shaqiri.


Liverpool uwekezaji wao huo mkubwa kwenye kikosi umeleta matunda ambako kwa sasa kwenye Ligi Kuu England wanachuana na Manchester City kwenye mbio za ubingwa huku wakitinga pia kwenye nane bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo watamenyana na FC Porto kwenye mechi ijayokuja.


Kocha Klopp amesisitiza kwamba ana furaha na kikosi alichokuwa nacho, hivyo hana mpango wowote wa kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha lijalo.


"Sidhani kama timu ilivyo kwa sasa itahitaji kufanya usajili mkubwa," alisema.


"Kitu pekee cha kufanya ni kujaribu kuliweka pamoja kundi hili la wachezaji na kujaribu kuboresha viwango tukiwa pamoja. Pengine yale matatizo yaliyokuwa ya Liverpool kipindi hicho, hayawezi kutokea kwa wakati huu."


Liverpool siku za karibuni imekuwa ikitajwa kuwinda huduma ya kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez sambamba na mchezaji Steven Bergwijn.


Post a Comment

0 Comments